Home Habari za michezo KISA KIPIGO CHA WATUNISIA….MASHABIKI YANGA ‘WAGUGUMIA NA UMBILIKOMO’ WA WACHEZAJI WAO…

KISA KIPIGO CHA WATUNISIA….MASHABIKI YANGA ‘WAGUGUMIA NA UMBILIKOMO’ WA WACHEZAJI WAO…

Mashabiki Yanga

Mchekeshaji maarufu nchini, Ulimboka Mwalulesa ‘Senga’ amesema licha ya Yanga kupoteza mechi yao ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Monastir, lakini ana matumaini timu hiyo itafanya vizuri katika mwendelezo wa michuano hiyo.

Yanga  ilianza vibaya michuano hiyo iliponyooshwa mabao 2-0 dhidi ya Waarabu hao ikiwa ni siku moja tangu watani zao Simba nao kuangushiwa kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Horoya kwenye ligi ya mabingwa Afrika, timu zote zikianzia ugenini.

Hata hivyo timu hizo zinatarajia kuwa nyumbani wikiendi hii, ambapo Simba atamkaribisha Raja Casablanca Jumamosi, huku Yanga wakishuka uwanjani Jumapili kuwapokea TP Mazembe.

Senga ambaye ni shabiki lialia wa Yanga, amesema licha ya kuumizwa na matokeo, lakini vijana walionesha soka safi wakicheza kwa kujiamini na kwamba anaamini mechi zinazofuata watatesa sana.

Hata hivyo mchekeshaji huyo hakusita kuwagusia watani zao Simba, akisema kuwa hata wao waliyakanyaga, hivyo hakuna wa kumcheka mwenzake kwani wote waliingia ‘motoni’.

“Tulichokosa sisi ni bahati tu kwa sababu kuna nafasi tulizipata kama mbili za Mayele na Aziz Ki, hata wale wenzetu (Simba) waliyakanyaga ila naamini mechi zinazofuata Yanga itaua,”

“Ninachojua kocha hataweza kuwaongezea kimo wachezaji ili warefuke kuhimili mipira ya juu, lakini kiufundi atakuwa ameona aboreshe wapi ili Jumapili hao Mazembe waweze kuacha pointi,” amesema mvunja mbavu huyo.

SOMA NA HII  GAMONDI AVUNJA UKIMYA HUU...NI KUHUSU ISHU YA PACOME..."ZOUZOUA AFUNGUKA HAYA