Home Habari za michezo KISA UCHAGUZI WA SIMBA JUZI…RAGE AMTUPIA JIWE LA GIZANI MO DEWJI…UJUMBE WAKE...

KISA UCHAGUZI WA SIMBA JUZI…RAGE AMTUPIA JIWE LA GIZANI MO DEWJI…UJUMBE WAKE HUU HAPA..

Habari za Simba

Baada ya uchaguzi wa Simba kutamatika na viongozi wapya kupatikana watakaoiongoza klabu hiyo kwa kipindi cha miaka minne ijayo.

Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage ametuma ujumbe mzito kwa mwekezaji ndani ya klabu hiyo Mohammed Dewji “Mo” ambae anamiliki hisa 49% za upande wa mdhanini.

Akizingumza Rage amesema;

“Wanachama na Mashabiki wa Simba tuheshimu uongozi uliochaguliwa ,tukubali waliochaguliwa ndio wameshinda Uchaguzi , Wameshindaje hiyo haituhusu ! tuache tofauti zetu tuwe kitu kimoja tuhakikishe Simba inafanikiwa”

“Kama Mohammed ananisikia sasa hivi , afanye mabadiliko makubwa sana kwenye upande wake, atuchagulie watu ambao wanatuheshimu , Mkutano wa juzi umepeleka fundisho kubwa sana kwenye maongezi ya Wanachama, hakuna Mtu anayempinga Mo Dewj, Mo tunamuhitaji kwa sababu anatusaidia mambo mengi sana”

“Sasa na yeye ili aweze kufanya kazi yake vizuri ahakikishe anapaya Watu , Maongezi ya Wanachama kwenye uchaguzi wa jana na ambavyo Watu wanaongea kwenye matawi ni hiyo hiyo”- amesema Rage.

SOMA NA HII  BIASHARA UNITED WANA BIASHARA NA SIMBA LEO