Home Ligi Kuu BIASHARA UNITED WANA BIASHARA NA SIMBA LEO

BIASHARA UNITED WANA BIASHARA NA SIMBA LEO


 BIASHARA United imeweka wazi kuwa leo ina biashara ambayo inahitaji kufanya mbele ya Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Karume, Mara.

Timu hiyo ambayo imepanda daraja msimu wa 2019 rekodi zinaonyesha kwamba imekutana na Simba mara sita na imekwama kusepa na ushindi mbele ya timu hiyo.

Ni mara tano Simba imeshinda na sare iliyopatikana ni moja kwa Wanajeshi hao wa Mpakani ambao wanashiriki mashindano ya kimataifa katika Kombe la Shirikisho.

Marwa Chamberi, Kocha Msaidizi wa Biashara United amesema kuwa Simba wanawachukulia poa Biashara United jambo ambalo wao hawalifikirii na badala yake wataonyesha kazi kwa vitendo.

“Sisi tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Simba na maandalizi yetu yapo vizuri kwa ajili ya kuona kwamba tunapata matokeo.

“Kikubwa ni kwamba tunahitaji pointi tatu muhimu hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kuwa bega kwa bega nasi,” amesema.

SOMA NA HII  MASAA YA MANULA KUBAKI SIMBA YAHESABIKA...DEWJI ASHINDWA KUTOA JIBU LA MOJA KWA MOJA...