Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA WAARABU…CAF WAZUIA ‘JANJA JANJA’ YA SIMBA…MSIMAMO WAO HUU HAPA..

KUELEKEA MECHI NA WAARABU…CAF WAZUIA ‘JANJA JANJA’ YA SIMBA…MSIMAMO WAO HUU HAPA..

Habari za Simba

Shirikisho la Soka Afrika CAF imegomea maombi ya klabu ya Simba ya kucheza saa 10 jioni mechi ijayo dhidi ya Raja Casablanca na sasa mchezo huo utachezwa saa 1 usiku.

Kwa mujibu wa kanuni za haki miliki kuanzia hatua ya Makundi mwenye maamuzi ya mwisho ni Kamati ya mashindano ya CAF.

Simba wanaikaribisha Raja Casablanca kutoka nchini Morocco na mchezo huo unatarajiwa kupigwa Februari 18 katika Dimba la Benjamin Mkapa.

Mchezo huo utakuwa ni mzunguko wa pili kwenye kundi hilo ambapo kwenye mzunguko wa kwanza, Simba walipoteza mbele ya Horoya kwa kufungwa goli 1-0, huku Raja Casablanca wakiifunga Vipers goli 5-0.

Simba na Raja Casablanca hazijawahi kukutana katika miaka ya hivi karibuni, huku takwimu za CAF zikiiweka Raja juu ya Simba kwa pointi nyingi zaidi.

Simba watashuka kwenye mchezo huo wakiwa na rekodi nzuri ya kucheza na kupata matokeo mazuri kwenye uwanja wa Mkapa hali ambayo inawapa Simba hali ya kujiamini.

Kwa vyovyote itakavyokuwa Wanamsimbazi watahitaji kuibuka na ushindi kwa njia yoyote ile ili kuweka hai matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali ya klabu bingwa.

Kwa misimu ya hivi karibuni, Wekundu wa Msimbazi wamekuwa wakifuzu hatua ya robo fainali, ambapo msimu uliopita walifuzu hatua hiyo kwenye kombe la shirikikisho.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI