Home Habari za michezo KUHUSU CHAMA AU AZIZ KI….MANARA AANIKA NANI BORA ZAIDI YA MWENZAKE…

KUHUSU CHAMA AU AZIZ KI….MANARA AANIKA NANI BORA ZAIDI YA MWENZAKE…

Aliyekuwa Afisa Mhamasishaji katika klabu ya Yanga Haji Manara amesema wachezaji wawili Stephanie Aziz Ki na Clatous Chota Chama ni wachezaji wazuri lakini wanatofautiana uwezo ambapo Aziz Ki amemuacha mbali Chama Jr.

Manara ambaye mara kadhaa wakati alimsifia Chama nyota wa kimataifa wa Zambia kama mchezaji bora nchini Tanzania amemwelezea Aziz Ki kuwa mchezaji wa kipekee ambaye ana uwezo wa kufanya chochote uwanjani hata bila kumpa nafasi anayohitaji Chama.

“Chama ni mchezaji mzuri lakini anahitaji nafasi ili aweze kuwa bora, unapomtaja Aziz Ki haitaji umpe nafasi. Ukimpa nafasi atakufanya vibaya, hata usimpo nafasi utaona yeye ni hatari pia”, aliongea hayo Feb 09, 2023 wakati akiongea na Jahazi la Clouds FM.

Haji Manara amesema kuwa ni wazi wachezaji hao wawili wanaongeza ubora kwenye Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara lakini kwenye nani ni bora bado Aziz Ki atakuwa juu.

Kwa sasa Chama anakipiga kunako klabu ya Simba akiwa na asisti za goli 13 wakati Aziz Ki ambaye anachezea Yanga ana mabao 6 timu zote mbili zikiwa kwenye michuano ya kimataifa Wekundu wa Msimbazi wakiwa Ligi ya Mabingwa na Timu ya Wananchi wako Kombe la Shirikisho.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONYESHA 'MANJENJE' YAO....MAYELE NA PHIRI WATABIRIWA VITA ....LUNYAMILA ATAJA BORA KATI YAO...