Home kimataifa GUARDIOLA ASIKITIKA KINOMA KISA SARE

GUARDIOLA ASIKITIKA KINOMA KISA SARE


PEP Guardiola, Kocha Mkuu wa Manchester City amesema kuwa anajisikia vibaya kuona timu yake imeshindwa kupata ushindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Southampton.


City ambao ni mabingwa watetezi walimenyana na Southampton katika mchezo uliokamilika kwa ubao wa Uwanja wa Etihad kusoma 0-0 kwa timu zote mbili.
Hivi karibuni Guardiola alikuwa akitumia nguvu kubwa kuwashawishi mashabiki kuhudhuria uwanjani kwenye mchezo huo lakini timu yake ikaambulia sare na kusepa na pointi moja.
Kocha huyo amesema kuwa ni jambo baya kwa timu yake kushindwa kupata ushindi lakini anawataka mashabiki wasikate tamaa watafanya vizuri kwenye mechi zijazo.

“Sikusema jambo lolote baya kwenye mchezo dhidi ya Leipzig, nilisema kuwa tunacheza mchezo mgumu dhidi ya Saint’s na tunahitaji matokeo, sikusema nani alikuja uwanjani nani hakuja.

“Kila siku nimekuwa nikisjikia vibaya ninapoona mambo hayaendi vizuri lakini nataka kuwahakikishia mashabiki kuwa waje uwanjani,” amesema.
SOMA NA HII  RASMI...ZIDANE KUPISHANA NA POCHETTINO PSG....AITWA CHAP QATAR KUMALIZANA NA MATAJIRI...