Home news MANARA AKOLEZA ‘CHUMVI’ ISHU YA UFUPI WA MABEKI WA YANGA…ANG’ANG’ANA NA DICKSON...

MANARA AKOLEZA ‘CHUMVI’ ISHU YA UFUPI WA MABEKI WA YANGA…ANG’ANG’ANA NA DICKSON JOB…

Habari za Yanga

Baada ya baadhi ya wachambuzi wa mpira nchini kusemankuwa magoli ya waliyofungwa @yangasc dhidi ya @us_monastir umesababishwa na ufupi wa mabeki wa Yanga.

Msemaji wa @yangasc ambae kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka miwili cha kutojihusisha na soka @hajismanara kupitia ukurasa wake wa instagram amewajibu wachambuzi hao kwa kuandika.

“Job nisikilize mimi, hakuna wa kukutoa relini ikiwa sie tupo,,na tushajua wengine walitaka uwe Meneja wao kabla ya kuja Yanga, baada ya kuwakatalia ndio lugha za chuki kwako.

Ufupi au Urefu haujawahi kuwa suluhisho la team kufungwa magoli ya Set Pieces duniani, ni Mtu mpumbav tu anaemini Yanga jana imefungwa magoli mawili Kwa sababu ya vimo.

El Mereikh kafungwa Goli la Set pieces wiki hii ktk ligi ya mabingwa,,Je Mabeki wao ni wafupi? Weekend hii pia,,Fc Lupopo,Piramides,Vipers wamefungwa magoli mawili kila mmoja ya mipira iliyokufa ,,hao nao ni Kwa sababu ya ufupi?

Mazembe na Team yao ya Makolo inayowapa laki laki za kula wamepasuliwa pia Kwa aina hyo ya Magoli, je kina Inonga na Babu Onyango ni Wafupi? It’s all about timing nyie kuku, ni lack of concentration,,ufupi au urefu wako hauhusiani, This is the football na sio Basketball hii, mnajitia ujuaji kumbe hamjui lolote baraka ya njaa njaa tu.

Mnamjadili kijana wa Watu kutwa kucha kisa ufupi wake,,Kuna Goli gani kahusika nalo jana? Acheni chuki Kwa hawa vijana,,duniani hajawahi kufanikiwa mtu kwa kutaka kumponda mwenzie.

Mmekataliwa Umeneja na Uwakala ,sasa unataka kumharibia dogo maisha,,wakati ww mwenyewe umeshayachezea na uzee ushakuvaa,,,njaa imeshtadi,,halaf unalazimisha ufupi wa binadamu mwenzio kama silaha,,

Onyo, Nitukaneni mm sio mchezaji wangu,,Ndegelec

@jobdick05″ amesema Manara.

SOMA NA HII  KUELEKEA KUANZA KWA LIGI KUU...NABI AMNYOOSHEA KIDOLE SHABANI DJUMA...ADAI HAKUWA BORA ...ALIKUWA KIBONGE...