Home Habari za michezo KISA VICHAPO VYA SIMBA NA YANGA …SMG AIBUKA NA HAYA MAPYA…WAKIZINGATIA WAMEULA…

KISA VICHAPO VYA SIMBA NA YANGA …SMG AIBUKA NA HAYA MAPYA…WAKIZINGATIA WAMEULA…

Simba na Yanga

Staa wa zamani wa Simba na Yanga, Said Maulidi ‘SMG’ amesema kitu pekee kinachoweza kuzisaidia klabu hizo kutoboa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni mifumo ya wakati sahihi na inayoendana na mashindano hayo.

Amesema kwamba michuano hiyo inachezwa kimbinu, hivyo Simba na Yanga, zisicheze mechi hizo kwa mazoea na wakuzichukulia poa timu pinzani.

“Kwa tathimini yangu tunakosa mbinu za mchezo husika na michuano husika kwa kuangalia vitu vya nyakati zilizopo ili kuweza kupata matokeo yanayotakiwa, kwa maana ya zisitumike mbinu zinazotumika kushindana ligi ya ndani;

Ameongeza; “Simba kwenye mchezo wao walitengeneza nafasi na kumiliki mpira ila ikashindikana kwenye kuzitumia, Yanga ilimiliki mpira na pasi nyingi ambazo hazikuzaa matunda, hivyo lazima kucheza kwa akili na siyo sifa zisizo na faida.”

Ametoa ushauri kwa timu hizo kwamba TP Mazembe inayocheza na Yanga na Raja Casablanca inayocheza na Simba,zimeshinda mechi zao za kwanza kwa mabao mengi ambayo ni ishara kwa mabeki kujipanga kuwakabiri.

“Yanga na Simba zinakutana na timu zenye wastani mzuri wa kufunga na zinajua kutumia nafasi, hivyo mabeki wapate muda wa kuzifuatilia na kujua namna ya kukabiliana nao.

Ameongeza “Ninachoshauri zitumie vyema uwanja wa nyumbani na zipotangulia kupata bao basi zilinde ushindi huo, zikijua ni mechi za kusaka pointi,”

SOMA NA HII  DABI YA WANAWAKE....YANGA PRINCESS 'WAIKUNYUGA' SIMBA QUEENS...WAFUTA UTEJA...