Home Habari za michezo MANARA : MASHABIKI SIMBA WANAMKOSEA BOCCO…JAPO SIWEZI KUMUOMBEA MEMA HATA KIDOGO…

MANARA : MASHABIKI SIMBA WANAMKOSEA BOCCO…JAPO SIWEZI KUMUOMBEA MEMA HATA KIDOGO…

Habari za Simba SC

Kutoka kwenye page ya Manara.

Naandika kama Mwanahabari mbobezi wa football nchini.

Kuna Vitu vinaumiza sana kuona Mchezaji kama huyu hapewi heshma yake na Washabiki wasiojua kitu wa Simba, team yao ikifanya vbaya Bangusilo wao ni Captain wao @john_22_bocco

Ni Upuuzi ni kutowapa respect Wachezaji waliofanya makubwa katika Soka nchini, ni Zaid ya Undumilakuwili na kukosa heshma kunakofaa kukemewe.

Katika kizazi hiki cha sasa, Nani kafunga kumzidi yeye nchi hii katika Premie league? Mpeni heshma anayostahili huyu Mtu, Tukiwa wote pale kashinda vikombe vingapi kama Captain?

Kwangu mimi hata Kocha wenu kumtoa juzi na Waarabu ni uchale wake tu, uwepo wake uwanjani siku ile ndio ulikuwa unafanya hata mpira ukae kule mbele na aliwapa tabu sana mabeki , ni kama kakariri zile Substitutions zake za michongo.

Hakuna kitu sikipendi na siwezi kukikalia kimya kama kuona heshma ya Wachezaji inanajisiwa , tena Wanajisi wenyewe ni Watu wasiojua lolote kuhusu football, Watu ambao hata danadana mbili kupiga hawawezi.

Ipo hv Captain, Wewe ni Star na endelea kupuuza maneno yao, baki hvyo ulivyo na beba hzo lawama kama changamoto tu, potezea Mwamba.

Siwezi kukuombea mazuri wewe na wenzio mkiwa uwanjani na Team yenu , lakini kama rafiki yako nitaendelea kukuheshimu daily , Kwa unachoendelea kutoa Kwa ajili ya football ya nchi hii.

@john_22_bocco ????

SOMA NA HII  FEI TOTO HAKUNA KUPOA HUKO LIGI KUU