Home Uncategorized AZAM FC YAIPIGIA HESABU DODOMA JIJI FC

AZAM FC YAIPIGIA HESABU DODOMA JIJI FC


 VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam FC wameanza kuipigia hesabu Dodoma Jiji kuelekea kwenye mchezo wao wa ligi utakaochezwa Novemba 5, Uwanja wa Azam Complex.


Azam FC ikiwa imecheza jumla ya mechi 9 imejikusanyia pointi 22 inakutana na Dodoma Jiji ambayo imecheza mechi 9 na kujikusanyia pointi 12 ikiwa nafasi ya 10.


Mchezo wao uliopita Azam FC ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya JKT Tanzania ikiwa nyumbani, Uwanja wa Azam Complex.


Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa kila kitu kipo sawa na wanaamini watapata pointi tatu mbele ya wapinzani wao.


“Siku zote uwanja wa nyumbani ni sehemu ambayo wachezaji wetu hucheza kwa kujiamini na kufurahi hasa kwa kuwa wanapata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki.

“Kikubwa ni kuendelea kupambana na kuona namna gani jambo letu litatimia kwa msimu huu wa 2020/21, mashabiki waendelee kutupa sapoti,” amesema.


Timu ambazo zilipita Uwanja wa Azam Complex na kupoteza ilikuwa ni pamoja na Mwadui FC, Coastal Union, Polisi Tanzania.

SOMA NA HII  MATOKEO YA LEO YAPO NAMNA HII, HAO MBAO NI BALAA WAISHUSHA NDANDA