Home Simba SC GOMES ATAJA KAZI YA BOCCO, MUGALU NA KAGERE KWA YANGA

GOMES ATAJA KAZI YA BOCCO, MUGALU NA KAGERE KWA YANGA


 DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amewataka washambuliaji wake watatu kuweza kufunga kwenye mchezo wao ujao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Simba ni mabingwa watetezi wa taji hilo ambapo wanakumbuka kwamba walisepa nalo msimu uliopita baada ya kushinda mbele ya Namungo FC kwenye fainali iliyochezwa Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga.

Itakutana na Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ambapo kwenye mchezo wao wa ligi uliopita ubao ulisoma Simba 0-1 Yanga ni bao la Zawad Mauya liliamua matokeo hayo.

Gomes amesema:”Tuna mchezo mgumu kwenye kombe la Shirikisho ila tupo tayari kwa ajili ya kuona kwamba tunapata matokeo kikubwa ni kila mmoja kuweza kutimiza majukumu yake.

“Kwa upande wa washambuliaji ambao wapo Bocco, (John), Mugalu, (Chris) na Kagere, (Meddie) wote ni washambuliaji wazuri na huwezi kuwaelezea kwa mmojammoja lakini ambacho ninahitaji ni kuona kwamba wanafunga.


“Tunahitaji kupata ushindi na kila mchezaji hilo anajua hivyo muhimu ni kuona mashabiki wanajitokeza kwa wingi kutupa sapoti,” amesema.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Julai 25, Kigoma.

SOMA NA HII  DABI YA KARIAKOO NGUMU KUMEZA,MANARA APATA KIGUGUMIZI