MANCHESTER United wamemkomalia kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Paul Pogba licha ya yeye mwenyewe kutaka kusepa kikosini hapo.
Pogba amesema kuwa kwa sasa anahitaji kupata changamoto mpya nje ya Premier League baada ya kucheza ndani ya Manchester United kwa muda wa miaka mitatu.
United wamesema kuwa watamuongezea posho na mshahara mchezaji huyo ili kupata huduma yake.