Home Habari za michezo NABI ATUMIA UMAFIA WA KIZUNGU KUIFUKUNYUA US MONASTIR…YANGA KESHO NI BIRIANI TU…

NABI ATUMIA UMAFIA WA KIZUNGU KUIFUKUNYUA US MONASTIR…YANGA KESHO NI BIRIANI TU…

Habari za Yanga SC

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi alikuwepo kwenye dimba la Stade Ahmed Khouaja, mjini Tunis akishuhudia mchezo wa Ligi Kuu kati ya wapinzani wao US Monastir wakiwa ugenini dhidi ya Rejiche, ambapo walishinda 2-0, mabao yake yakifungwa na Idrissa Mhirsi dakika 10 na Bassam Deli dakika ya 30.

Nabi pia alifanikiwa kushuhudia mchezo mwingine kabla ya huo kwenye Ligi wakati Monastir walipofungwa bao 1-0 na Ben Guerdan kwenye uwanja wa Mustapha Ben Jannet.

Yanga watakuwa ugenini kusaka pointi tatu muhimu katika mchezo wao huo utakaopigwa, Uwanja wa Olympique Hammadi Agrebi, katika mji huo mkuu wa Tunisia.

Akizungumza nasi, Nabi alisema amepata muda mzuri wa kuwatazama wapinzani wao Monastir katika michezo miwili waliyocheza kwenye ligi hiyo na kuona ubora na madhaifu yao.

Alisema amewaona wachezaji hatari ambao wanatakiwa kuwachunga na sehemu gani wako bora na wataingia katika mchezo wao wa kwanza wa hatua ya makundi kwa tahadhari kubwa.

“Tumeona ubora wa kikosi cha wapinzani wetu kwa kushuhudia michezo yote miwili ya ligi kuu nchini humu, wachezaji gani ni hatari na wanaotakiwa kuchungwa tunapokutana nao,” alisema Nabi wakati akizungumza na gazeti hili kutoka nchini Tunisia.

Alisema baada ya mechi yao na Namungo FC waliangalia wapi panapohitajika kuimarishwa na kufanyia kazi mapungufu yao ikiwemo sehemu ya kiungo.

“Tumefanya maandalizi mazuri tunatambua mchezo utakuwa wa ushindani mkubwa kwa sababu tuko ugenini na tunahitaji kupata alama katika mchezo wetu huo wa kwanza katika hatua ya makundi,” aliongeza.

Kikosi cha Yanga kipo jijini Tunis kikiwa kimefikia kwenye Hotel ya nyota tano ya Golden Tulip tayari kwa ajili ya mchezo wao huo wa Jumapili.

SOMA NA HII  MTANGAZAJI:- YANGA ISIPOKUWA MAKINI ITAPIGIKA NA SIMBA SC...TANO ALIFUNGWA ROBERTINHO SIO BENCHIKHA