Home Habari za michezo SAA CHACHE KABLA YA KUKIPIGA NA HOROYA..MASTAA SIMBA WAWEKEWA MIL 100 ZA...

SAA CHACHE KABLA YA KUKIPIGA NA HOROYA..MASTAA SIMBA WAWEKEWA MIL 100 ZA USHINDI..

Habari za Simba

Mabosi wa Simba katika kuhakikisha wachezaji wanapata mzuka na motisha ya kutosha ili kupata matokeo mazuri kwenye mechi hiyo wamemwaga mkwanja wa kutosha ambao hata hivyo umefanywa siri,

Wachezaji wote wa Simba ukiachana na wanne wapya waliosajiliwa kwenye dirisha dogo kila mmoja alipokea bonasi yake aliyostahili kupata baada ya kikosi hicho kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Bonasi hizo zimelipwa ili kuongeza motisha kwa wachezaji kwani kila mmoja alionekana kuwa na furaha baada ya kupata pesa hizo walizokuwa wanazisikilizia tangu Simba ilipotinga hatua ya makundi kwenye michuano hiyo mikubwa ngazi ya klabu Afrika.

Inaelezwa kwenye mazoezi ya juzi asubuhi kabla ya kikosi kuondoka nchini wachezaji walionekana kuwa na furaha na mzuka mkubwa huku kila mmoja akiwa na morali ya kutaka kufanya vizuri kwenye mchezo huo wa kwanza hatua ya makundi ugenini.

Kama halikutosha hilo wachezaji wa Simba walielezwa utaratibu wa bonasi kwenye Ligi ya mabingwa upo vile vile katika michezo ya nyumbani pamoja na ile ya ugenini kama watakuwa wamepata ushindi au sare.

Wachezaji wa Simba kama wakipata ushindi mechi na Horoya bonasi itatoka Sh100 milioni na watagawana wote kama wakipata sare watapata chini ya hiyo wakipoteza hawataambulia chochote.

SOMA NA HII  SAMATA AKAMATIKI TENA REKODI ZAKE NI ZAIDI YA HISTORIA

1 COMMENT