Home Azam FC AZAM FC YAILAMBA IHEFU GOLI 3-0

AZAM FC YAILAMBA IHEFU GOLI 3-0

 


Wakati mechi baina yao ikmalizika katika Uwanja wa Azm Complex, Azam FC inazidi kuiweka pabaya Ihefu SC kutokana nakukubali kichapo cha goli  3-0.

Ikionekana kuwa na uchu wa kuibuka na ushindi katika mchezo huo, Azam iliuanza mchezo kwa kasi ikilishambulia kama nyuki lango la Ihefu ambayo ilionekana kucheza kwa kujilinda katika dakika za mwanzoni.

Harakati hizo za Azam FC zilizaa matunda mapema katika dakika ya tisa baada ya kupata bao la utangulizi lililofungwa na mshambuliaji Iddi Selemani ‘Nado’

Nado alifunga bao hilo kwa kichwa akiunganisha krosi iliyochongwa kutoka upande wa kulia na beki Abdul Hamahama.

Mara baada ya kufungwa bao hilo, Ihefu walionekana kufunguka na kuanza kupishana na Azam ingawa walikosa makali katika safu ya ushambuliaji na kushindwa kuwa na madhara katika eneo la ulinzi la wapinzani wao.

Matokeo hayo yalidumu hadi pale refa Hance Mabena kutoka Tanga alipopuliza kipyenga cha kuashiria mapumziko.

Kipindi cha pili kilianza kwa Ihefu kuwatoa Shaban Iddy na Issah Ngoah ambao nafasi zao zilichukuliwa na Joseph Mahundi na Joseph Kinyozi

Mabadiliko hayo yalionekana kuipa uhai Ihefu SC lakini dakika sita tu baada ya kipindi cha pili kuanza, Ayoub Lyanga aliwapatia Azam bao la pili kwa shuti kali la mguu wa kushoto akimalizia pasi ya Nado.

Iddi Nado aliifungia tena Azam FC goli la tatu na la mwisho katika dakika ya 92 hivyo kutamatisha mchezo huo kwa kuifanya Azam FC kusalia katika nafasi ya tatu ikiwa na jumla ya alama 44 huku ikiwa imecheza michezo 24.

SOMA NA HII  FT: AZAM FC 2-3 YANGA SC.......SOPU AMSOPOA DIARRA MAR TANO...