Home Uncategorized RASMI NYOTA WA YANGA ATEMWA MAZIMA

RASMI NYOTA WA YANGA ATEMWA MAZIMA


UONGOZI wa Azam FC umethibiisha kuachana rasmi na nyota wa zamani wa Yanga, Donald Ngoma, baada ya mkataba wake kufikia ukingoni Juni 14.


Ngoma alijiunga na Azam FC akitokea Klabu ya Yanga ambapo aliweza kutwaa Kombe la Mapinduzi mwaka jana na Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) msimu uliopita.

Kwa kipindi chote cha misimu miwili, alichodumu ndani ya Azam FC, Ngoma amekuwa mmoja ya washambuliaji wa kutumainiwa akiwa mfungaji bora wa timu yetu msimu uliopita kwa mabao yake 14 aliyoifunga kwenye mashindano yote.

Hadi anamaliza mkataba wake kwenye timu hiyo yenye maskani yake Azam Complex, Chamazi, Ngoma amefanikiwa kucheza jumla ya mechi 42 za mashindano yote, akihusika katika mabao 20, baada ya kufunga 16 na kutoa pasi za mwisho nne.

SOMA NA HII  MASHABIKI TUENDELEE KUJITOKEZA UWANJANI KUZIPA SAPOTI TIMU