Home Uncategorized YANGA KAMILI GADO KUVAANA NA JKT TANZANIA

YANGA KAMILI GADO KUVAANA NA JKT TANZANIA


BAADA ya kusepa na pointi tatu mbele ya Mwadui FC kwa ushindi wa bao 1-0, tayari Yanga imeanza kujiandaa kwa ajili ya mchezo wake wa kesho dhidi ya JKT Tanzania.

Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael ilianza mazoezi yake kwenye Uwanja wa Shule ya John Maelini jijini Dodoma.

Mchezo huo utapigwa kesho, Juni 17 Uwanja wa Jamhuri majira ya saa 10:00.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Mkwassa amesema kuwa wapo tayari kwa ushindani.

Yanga ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 28 kibindoni ina pointi zake 54.

SOMA NA HII  YANGA YA KAZE KAZINI LEO KUTESTI MITAMBO