Habari za Simba
Habari za michezo

KISA MECHI YA VIPERS NA SIMBA…KIBU DENIS KUWA NNJE KWA WIKI MOJA…ISHU NZIMA IKO HIVI….

admin March 3, 2023 1:09 pm

Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Kibu Denis atakuwa nje ya uwanja kwa takriban wiki moja kutokana na majeraha aliyoyapoata katika mchezo uliopita wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vipers.

Daktari wa timu hiyo, Edwin Kagabo amesema Kibu amepata maumivu ya mguu na baada ya vipimo anahitajika kuwa nje kwa muda wa wiki moja ili kupona kabisa.

“Kibu amepata maumivu kwenye mchezo uliopita dhidi ya Vipers, haikuwa mbaya sana lakini inabidi akae nje ya uwanja kwa wiki moja kabla ya kuanza mazoezi,” alisema Dk Edwin.

Simba inatarajia kushuka dimbani kesho kwenye mchezo wa Uhuru katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam hatua ya 16 Bora dhidi ya African Sports na kisha, Marchi 7, 2023 watawakaribisha Vipers kutoka Uganda kwenye Ligi ya Mabibigwa Afrika.

UKWELI MCHUNGU….KWA SIMBA HII YA ‘WACHOVU’ WENGI…HUENDA TAIFA LIKAPATWA NA AIBU KWENYE CAF SUPER LEAGUE.. KUHUSU ISHU YA KUPEWA UKOCHA TAIFA STARS….NABI AANIKA MUSTAKABALI WAKE NA YANGA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply