Vipers muda wowote asubuhi hii watatua Dar kuja kuwakabili Simba SC, mchezo wa mzunguko wa nne, hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.
Vipers walipoteza mchezo wao nyumbani Uganda dhidi ya Simba na sasa wanakuja ugenini.
Sasa kocha wa Vipers Beto Bianchi amefichua baada ya kuisoma Simba mbele ya Waarabu ameamua kubadili mfumo kwa timu hiyo kisha kuwalisha nyota wake mbinu za kuimaliza Simba kesho Kwa Mkapa kama ilivyonyooshwa na Raja.
βKesho tutakuwa na mifumo mingi na italenga maeneo yote kuanzia safu ya ulinzi hadi ushambuliaji, sihitaji kuona Vipers inakuwa timu ya mwisho tutafanya kama Raja Casablanca kushinda ugenini.β amesema Bianchi