Home Habari za michezo MCHAMBUZI: UTEUZI WA MO DEWJI NDANI YA SIMBA NI BATILI…KATIBA HAITAMBUI ALICHOFANYA…

MCHAMBUZI: UTEUZI WA MO DEWJI NDANI YA SIMBA NI BATILI…KATIBA HAITAMBUI ALICHOFANYA…

Habari za Simba SC

Mchambuzi Abdulaziz Mrisho akizungumzia uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC uliofanywa na mwekezaji Mohammed Dewji kupitia TBC amesema hakuna kifungu Kisheria na kikatiba kinachompa Mo mamlaka ya kumteua Try Again.

Amebainisha kuwa wajumbe 8 huiwakilisha Simba SC kwenye Bodi ya Wakurugenzi, ambapo wajumbe 6 huchaguliwa na wawili wa huteuliwa ambapo mmoja kati yao atachaguliwa kama Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi. Hapa ndipo unaona mwenye mamlaka ya kumchagua Try Again ni Murtaza Mangungu na sio Mo Dewji.

“Katiba ya Simba Ibara ya 27 inampa mamlaka Mwenyekiti Simba SC aliyechaguliwa na Wanachama kuteua mjumbe wa bodi miongoni mwa upande wa asilimia 51 ambaye ni Salim Try Again baada ya hapo akapewa nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi.”

“Kikatiba hakuna kifungu kinachompa mamlaka Mohammed Dewji kuteua Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba anachaguliwa na wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi wa klabu.”

Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC ndio yenye mamlaka ya kupitisha nani awe Mwenyekiti. Kitendo cha Mo kumteua Try Again kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC hakipo kisheria na kikatiba.

SOMA NA HII  YANGA YATEKETEZA BILIONI 1.1 KWA NYOTA 7, PHIRI KUJA SIMBA, NDANI YA CHAMPIONI