Rais wa Heshima wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ amesema kuwa amemsamehe aliyewahi kuwa Msemaji wa Klabu hiyo, Haji Manara kufuatia matusi ambayo amekuwa akimtukana mitandaoni baada ya kuondoka katika klabu hiyo.
Mo Dewji ametoa kauli hiyo wakati akihojiwa na Global TV Online kuhusu adha anayoipata kufuatia kauli za Manara kuhusu Mo Dewji na viongozi wa Simba kwa ujumla.
“Huyu ndugu yetu tumefanya naye kazi vizuri, najua amekuwa
akinitukana na ananitukana lakini mimi nimemsamahe kwa sababu maisha ni mafupi, hayo yamepita hata kama akiendelea kunitukana mimi nimemsamehe.“Na si yeye tu, kuna wengine pia ambao wamenisema vibaya, na kunitukana. Mimi ni aina ya mtu ambaye siweki chuki ndani ya moyo wangu. Mungu amenijalia vitu viwili, kwanza sina wivu na mtu na pili sibaki na kinyongo, likitokea jambo mimi nasamehe na ninamwachia Mungu.
“Ikitokea siku moja amekuja kuomba msamaha mimi kusema ukweli sikuwa na shida na Haji Manara, tumetofautiana kwenye maono, kwenye shabaha ya Simba, hapo ndipo tulipoishia. Mimi sina shida naye, tayari nishamsamehe na kunitukana kwangu wala hainipi shida yoyote.,” amesema Mo Dewji.