Wakati mara kadhaa ikisemwa Rais wa Heshima wa Klabu ya Simba Mohamed Dewji anajifaidisha na Simba SC, hali ni tofauti kwa Mwekezaji huyo anaemiliki 49% ya hisa za Klabu ya Simba.
Akijieleza Mo Dewji katika Mahojiano aliyofanya na Global TV anasema;
“Ukiniambia Simba ni Biashara kwangu Hapana, ni Hasara kwangu ndiyo, kifedha inanipa hasara, Kuna wafadhili wengi sana ambao wamekuja na wamepita wengi wao wamefilisika Kutokana na kuwekeza au kufadhili Simba na Yanga,”
Mo Dewji ndio mwekezaji wa Klabu hiyo kwa sasa akiwa na umiliki wa 49% ya hisa za klabu huku wanachama wakiwa na 51%.
Katika uwekezazji huo, Mo Dewji aliweka hadharani hundi yenye thamani ya Bil 20 , ambapo pia alibainisha kutumia zaidi ya Bilioni 21 kwa miaka minne iliyopita ikiwa ni nnje ya Bil 20 alizotoa.
Toka kuwa mwekezaji wa timu hiyo, Wekundu hao wa Msimbazi wamefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali mara nne, huku wakichukua ubingwa mara nne mfululizo kabla ya Yanga kuwazuia msimu uliopita.
Mo unatuvuruga mzee, huu si wakati wa hoja hiyo. Twende kwanza tumalize mashindano yote ambayo tunashiriki ilitujue tumepata nini na tume kosa nini, swala la faida au hasara tulijadili wakati hatuko katika mashindano yoyote na timu iwe imeshakamilisha usajili kwaajili ya msimu ujao wa 2023/24. Kuibua mjadala wa faida na hasara wakati huu ni kuiondoa timu kwenye njia, unaharibu concentration ya timu, bench la ufundi, na kuondoa umoja na mshikamano miongoni mwa wanachama na mashabiki wa timu. Naomba nimuombe na kumshauri ndugu yangu Mo swala hili aliache kwanza ilitupambane katika robo fainali na NBC PRIMIER LEAGUE tukiwa wamoja. Kama Kuna changamoto yoyote basi MO aangalie namna bora ya kuwasilisha kwa Mamlaka zilizo ndani ya klabu au tuitishe kikao Cha dharura Cha wanachama wote. Naomba pia vikao vya wazee virejeshwe ilikupata busara zao kila tunapokabiliana na changamoto iwe Ni mechi au maswala ya ndani ya timu. Tafadhali sana ndugu MO na wanasimba kwa ujumla. Naamini siwezi kuwa muasi kwa mawazo yangu haya. Simba nguvu moja.