Kumekuwa na stori nyingi kwenye mitandao ya kijamii kuwa Yanga itawakosa wachezaji wake wengi kwenye mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe nchini Congo.
Hii inatokana na kile kinachoelezwa kuwa ni kutokana na kupata kadi mbili za njano katika michezo miwili inayofuatana ya michuano hiyo.
Kwa mujibu wa kanuni za mashindano ya CAF, mchezaji atakosa mchezo unaofuata kwa kupata kadi mbili za njano mfululizo.
Kwa Yanga Djuma Shabani pekee ndiye aliepata kadi mbili za njano katika mechi mbili zilizofuatana, alipata kadi katika mechi ya Real Bamako katika Dimba la Mkapa na mchezo dhidi ya Us Monastir.
Mchezaji mwingine aliyepata kadi ya njano katika mchezo wa Bamako ni mshambuliaji Kennedy Musonda ambaye mchezo wa pili hakupata kadi.
Lakini katika mchezo wa wikiendi iliyopita kati ya Yanga na Maonastir, wachezaji wa Yanga waliopata kadi ni wanne.
-Djigui Diarra
-Djuma Shabani
-Ibrahim Bacca
-Khalid Aucho