Home Habari za michezo KUHUSU SIMBA KUSHINDA GOLI 7-0 DHIDI YA HOROYA….EDO KUMWEMBE AFICHUA HAYA YA...

KUHUSU SIMBA KUSHINDA GOLI 7-0 DHIDI YA HOROYA….EDO KUMWEMBE AFICHUA HAYA YA NYUMA YA PAZIA…

Habari za Simba

Simba ilijikatia nafasi ya kufuzu kwa hatua ya Robo Fainali juzi jumamosi baada ya kuitandika Horoya mabao 7-0 kaika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Ushindi huo umegeuka gumzo mitaa ya msimbazi lakini mchambuzi nguli wa michezo nchini, Edo Kumwembe amewatahadharisha Simba kutobweteka na ushindi huo na matokeo yake wajipange kwa hatua inayofuata ambayo ametanabaisha kuwa ni ngumu zaidi.

Akizungumza Edo anasema;

“Kwa Horoya ilikuwa rahisi kwa Simba kufanya kila walichotaka uwanjani kwa sababu wapinzani wao walionekana kuwa dhaifu na hawakuwa na mipango madhubuti. Hata katika pambano la kwanza kule Conakry, Simba hawakustahili kupoteza pointi tatu kama kina John Bocco wangekuwa makini”.

Lakini sasa wanaenda kukutana na timu kali zaidi (Robo Fainali) Wanaweza kulitumia pambano la marudiano dhidi ya Raja pale Casablanca kama mfano wa namna wanavyoweza kucheza na timu kubwa katika hatua inayofuata (Robo)”

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO MABOSI YANGA WALIVYOZIMA NDOTO YA SIMBA KUMUIBA NABI ...ALIWEKEWA MKATABA MNOO NA MO DEWJI...