Habari za Simba
Habari za michezo

KUHUSU SIMBA KUSHINDA GOLI 7-0 DHIDI YA HOROYA….EDO KUMWEMBE AFICHUA HAYA YA NYUMA YA PAZIA…

admin March 27, 2023 7:55 pm

Simba ilijikatia nafasi ya kufuzu kwa hatua ya Robo Fainali juzi jumamosi baada ya kuitandika Horoya mabao 7-0 kaika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Ushindi huo umegeuka gumzo mitaa ya msimbazi lakini mchambuzi nguli wa michezo nchini, Edo Kumwembe amewatahadharisha Simba kutobweteka na ushindi huo na matokeo yake wajipange kwa hatua inayofuata ambayo ametanabaisha kuwa ni ngumu zaidi.

Akizungumza Edo anasema;

“Kwa Horoya ilikuwa rahisi kwa Simba kufanya kila walichotaka uwanjani kwa sababu wapinzani wao walionekana kuwa dhaifu na hawakuwa na mipango madhubuti. Hata katika pambano la kwanza kule Conakry, Simba hawakustahili kupoteza pointi tatu kama kina John Bocco wangekuwa makini”.

Lakini sasa wanaenda kukutana na timu kali zaidi (Robo Fainali) Wanaweza kulitumia pambano la marudiano dhidi ya Raja pale Casablanca kama mfano wa namna wanavyoweza kucheza na timu kubwa katika hatua inayofuata (Robo)”

KUHUSU ISHU YA NABI KUSEPA YANGA….MAZITO YAIBUKA…KIGOGO JANGWANI AANIKA A-Z JAMBO LILIVYO… KISA KIPIGO CHA GOLI 7-0….BEKI HOROYA AENDELEA KUWEWESEKA NA JINA LA CHAMA…AFUNGUKA ALIVYOTESWA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply