Home Habari za michezo SIMBA SC YAWAFATA RAJA CASABLANCA KIMAFIA…WACHEZAJI WAKOSA TIKETI ZA NDEGE

SIMBA SC YAWAFATA RAJA CASABLANCA KIMAFIA…WACHEZAJI WAKOSA TIKETI ZA NDEGE

SIMBA SC YAWAFATA RAJA CASABLANCA KIMAFIA...WACHEZAJI WAKOSA TIKETI ZA NDEGE

MASTAA wa Simba wasiokuwepo timu za taifa wanaendelea kujifua na mazoezi ya mwisho leo asubuhi kabla ya kuanza safari ya kwenda nchini Morocco, huku mabosi wa klabu hiyo wakiweka mikakati ya kuifuata Raja Casabalanca kwa mafungu kati ya kesho na keshokutwa wakipanga kumaliza makundi ya Ligi za Mabingwa Afrika kwa heshima.

Simba na Raja zimeshafuzu robo fainali ya michuano hiyo kupitia Kundi C, zitakutana Jumamosi katika mechi ya kukamilisha ratiba, huku Wekundu wakiwa na kumbukumbu la kuchapwa mabao 3-0 nyumbani kwenye mchezao wa kwanza.

Mabosi wa Simba katika kuhakikisha wanaenda kuweka heshima ugenini imepanga kuondoka mapema leo ili kuwahi mchezo huo baada ya kubaini kuna tatizo la usafiri kwenda Morocco.

Habari kutoka ndani ya Simba kimelidokeza SOKA LA BONGO kuwa kikosi cha timu hiyo kinatarajia kuondoka kwa mafungu, huku msafara wa kwanza ukianza kuondoka leo na ule wa mwisho utaondoka Jumatano na mastaa waliopo timu nyingine za taifa nje ya Tanzania wataunga huko huko.

“Timu itaanza kuondoka Jumanne na baadhi ya wachezaji na wengine watafuata Jumanne hii ni kutokana na changamoto iliyopo kuna wachezaji wapo timu ya taifa wana mechi ikiwamo wale wa Taifa Stars dhidi ya Uganda hivyo hao wataungana na wenzao baada ya kukamilisha ratiba ya timu zao za taifa,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;

“Mchakato wa ukataji wa tiketi umekamilika uongozi umefanya majukumu yao kilichobaki ni maandalizi na timu kuanza safari kwaajili ya mchezo huo ambao utacheza Aprili mosi kwa upande wa Morocco lakini kwa Tanzania ni saa nne usiku Machi 31.”

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu alipotafutwa alithibitisha juu ya mipango ya safari hiyo kwa kusema kuna changamoto ya usafiri anapambana kutafuta tiketi ambazo amekiri kuwa wana asilimia kubwa ya kusafiti Machi 28 au 29.

“Napambana kusaka tiketi kuna changamoto ya usafiri lakini kuna asilimia kubwa timu kuondoka kati ya siku hizo mbili Jumanne au Jumatano.”

Akizungumzia maandalizi kwa ujumla alisema wachezaji wote ambao hawajapata nafasi ya kuitwa kwenye vikosi vya timu zao za taifa wameingia kambini na wanaendelea na mazoezi tayari kwa kujiweka fiti kuelekea mchezo huo.

“Wachezaji wote wapo kambini isipokuwa walio kwenye timu zao za taifa maandalizi kiujumla yanakwenda vizuri chini ya makocha wetu wote wawili mkuu na msaidizi na kiu ya kila mmoja ni kuona tunaopata matokeo mazuri ugenini baada ya kupoteza nyumbani,” alisema Rweyemamu.

SOMA NA HII  MAYELE PAMOJA NA MASTAA HAWA WA YANGA KUKOSEKANA KESHO DHIDI YA TZ PRISONS...