Home CAF BAADA YA KUONA MAJI YANAZIDI UNGA…ZAMALEK WAOMBA MSAADA CAF ILI WAFUZU ROBO...

BAADA YA KUONA MAJI YANAZIDI UNGA…ZAMALEK WAOMBA MSAADA CAF ILI WAFUZU ROBO FAINAL…

Zamalek

Klabu ya Zamalek ya Misri imetoa taarifa rasmi ya kupeleka malalamiko CAF kuhusu klabu ya Esperance ya Tunisia kumtumia mchezaji Houssem Dagdoug kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya Makundi msimu huu dhidi ya Al Merrikh wakati mchezaji huyo alifeli kwenye vipimo vya dawa zilizozuiliwa michezoni.

Houssem Dagdoug alitumiwa kwenye mchezo uliozikutanisha Esperance dhidi ya Al Merrikh ambapo Esperance ilishinda 1-0, Zamalek wanasema ushindi huo ni batili! hivyo klabu hiyo ya Misri wametazama maslahi yao endapo pinti tatu (3) walizopata Esperance dhidi ya Al Merrikh zitaondolewa!

Kwenye Kundi D, Esperance ndio vinara wakiwa na alama tisa (9), Belouizdad wana alama sita (6) wapo nafasi yapili na nafasi ya tatu wapo Zamalek wenye alama nne (4) sawa na Al Merrikh ambao wapo nafasi ya nne.

Zamalek wanaona ni bora Esperance inyang’anywe alama tatu (3) ibaki na alama sita (6) halafu Al Merrik ipewe alama hizo na kufikisha alama saba (7). Zamalek bado wana mchezo mmoja na Al Merrik nyumbani [Misri] kama wanashinda watafikisha alama saba (7)!

Kwa hiyo Zamalek wameamua kupiga hesabu za kiutu-uzima na kucheza nje ya uwanja.

SOMA NA HII  BAADA YA KUBWAGA MANYANGA, MANARA KUZUNGUMZA LEO