Home Habari za michezo CHAMA AIPA SIMBA MIL 160 ZA HARAKA HARAKA…..MO DEWJI ‘AVUNJA BANK’ KUWEKA...

CHAMA AIPA SIMBA MIL 160 ZA HARAKA HARAKA…..MO DEWJI ‘AVUNJA BANK’ KUWEKA MAMBO SAWA…

Simba vs Vipers
[the_ad id="25893"]

Mstaa wa Simba akiwemo Clatous Chama, katika mechi mbili zilizopita za Ligi ya Mabingwa Afrika Kundi C, wamevuna mkwanja mrefu ambao ni takribani shilingi milioni 160.

Ni ushindi wa nje ndani ambao Simba imeupata dhidi ya Vipers ambapo ilipokuwa Uwanja wa St Mary’s, Uganda, matokeo yalikuwa 0-1, ikisha Jumanne iliyopita pale Uwanja wa Mkapa, Dar, Simba ikashinda 1-0.

Katika mechi ya kwanza, mfungaji alikuwa Henock Inonga, kisha Chama ndiye aliyefunga bao hilo pekee.

Katika fedha hizo, shilingi milioni 10 ni ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Samia Suluhu ambaye aliahidi kutoa shilingi milioni 5 kila bao kwa timu ambazo zinashiriki mashindano ya kimataifa msimu huu, Simba na Yanga, hivyo mabao mawili waliyofunga Simba dhidi ya Vipers, yamewapa shilingi milioni 10.

Taarifa kutoka chanzo cha kuaminika, zimeeleza kuwa, mabosi wa Simba wakiongozwa na Rais wa Heshima wa klabu hiyo, Mohamed Dewji, nao wametoa jumla ya shilingi milioni 150 katika kuwapongeza wachezaji wa kikosi hicho.

“Ushindi wa mechi mbili dhidi za Vipers umeongeza furaha huku milioni 150 wakipewa wachezaji kutoka kwa wadau wakiongozwa na Mo Dewji, kuna zaidi ya hizo ambazo zitakusanywa mpaka wiki itakapoisha.

“Kikubwa ni kuwaongezea morali wachezaji ili wafanye vizuri kwenye mechi za kimataifa na malengo ni kutinga hatua ya robo fainali,” ilieleza taarifa hiyo.

SOMA NA HII  KISA SIMBA NA YANGA...WADHAMINI LIGI KUU WAIBUKA NA HOJA MPYA...WAWEKA WAZI VIAUMBELE VYAO...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here