Home Habari za michezo KESHO SIMBA NI KUSUKA AU KUNYOA….MBRAZILI AANIKA ANACHOKITAKA KWA MASTAA WAKE…

KESHO SIMBA NI KUSUKA AU KUNYOA….MBRAZILI AANIKA ANACHOKITAKA KWA MASTAA WAKE…

Habari za Simba

Kesho Alhamisi, Machi 2, 2023 kikosi cha Simba kina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya African Sports.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Uhuru kwa kuwa Uwanja wa Mkapa unafanyiwa maboresha na utatumika kwa mechi za kimataifa.

Simba inaingia kwenye mchezo huo ikiwa inakumbuka kwamba ilitinga hatua hiyo kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union.

Moja ya mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa na kila timu ilicheza kwa umakini huku Simba ikipata nafasi ya kufunga bao hilo kupitia kwa Sadio Kanoute, kiungo mgumu ndani ya kikosi hicho.

Tayari kikosi cha wekundu hao kimerejea Dar kikitokea Uganda kilipokuwa na kazi ya kusaka ushindi dhidi ya Vipers mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Robert Oliveira, Kocha Mkuu wa Simba ameweka wazi kuwa anahitaji ushindi kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Alhamisi.

SOMA NA HII  KLABU HII LIGI KUU YAANGAMIA...HALI NI TETE MAAJABU PEKEE NDIO YATAIKOMBOA...ISHU NZIMA IPO HIVI