Home Habari za michezo KOCHA US MONASTIR:- “TUMEFUZU… HATUTOTUMIA NGUVU NYINGI…TUKICHEZA NA YANGA

KOCHA US MONASTIR:- “TUMEFUZU… HATUTOTUMIA NGUVU NYINGI…TUKICHEZA NA YANGA

KOCHA US MONASTIR:-

Kocha Mkuu wa US Monastir, Darko Novic ametoa kauli ya kinyonge kuwa hawatatumia nguvu nyingi watakapovaana na Mabingwa wa Soka Tanzania Young Africans.

Miamba hiyo itakutana kesho Jumapili (Machi 19) katika mchezo wa mzunguuko watano wa Kundi D, Kombe la Shirikisho Barani Afrika, Uwanja wa Bengamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Kocha Darko Novic amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo huo, lakini hatatumia nguvu kubwa, kwani tayari wameshafuzu Robo Fainali hivyo hawatawatumia wachezaji wao muhimu na tegemeo kwa lengo la kupata majeraha wakati wana kibarua kigumu mbele ya safari.

“Hatukuja Tanzania kutafuta alama tatu wala suluhu kwa sababu tumeshafuzu Robo Fainali, hivyo tutacheza mpira wa kawaida bila ya kutumia nguvu nyingi kama tulivyocheza nao Tunisia.”

“Tunafahamu wapinzani wetu wanahitaji ushindi ili wafuzu hatua inayofuatia ya Robo, hivyo tayari nimewaambia wachezaji wacheze kwa makini ili wamalize mchezo huo bila ya majeraha yoyote.”

“Kwani tuna kibarua kigumu mbele ya safari ndefu katika michuano hii, malengo yetu ni kufika fainali hivyo sitaki kuona wakipatikana majeruhi katika mchezo huu,” amesema Darko Novic.

Wakati huo huo Kocha Mkuu wa Young Africans Nasreddine Nabi amesema: “Sitaki kuwaangalia wapinzani wangu nini wanachotaka kukifanya katika kuelekea mchezo huo.”

“Ninaendelea kukiimarisha kikosi changu ili kipate matokeo mazuri ya ushindi na sio kitu kingine, nimepanga kutumia wachezaji wangu wote muhimu ili kuhakikisha tunapata ushindi wa hapa nyumbani utakaotupeleka Robo Fainali,”

US Monastir tayari imefuzu Robo Fanaili ya Kombe la Shirikisho Afrika katika Kundi D ikiwa na alama 12, ikifuatia na Young Africans yenye alama 07, TP Mazembe ipo nafasi ya tatu ikiwa na alama 03 na AS Real Bamako ipo nafasi ya mwisho kwa kumiliki alama 02.

SOMA NA HII  TIKETI ZA KITONGA MECHI YA YANGA....TIKETI 1000 KUTOLEWA BURE...THAMINI UTU CHANGIA DAMU