Home Habari za michezo MANARA:- TFF HAWAJINIFUNGIA KUSEMA YANGA…KUNA WATU WANANIDHALILISHA SANA…

MANARA:- TFF HAWAJINIFUNGIA KUSEMA YANGA…KUNA WATU WANANIDHALILISHA SANA…

Habari za Yanga

Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara ametema nyongo kwa wachambuzi na waandishi wa habari za michezo wanaomzungumzia kila wakati na safari hii ameenda mbali na kuwageukia wamiliki wa vyombo hivyo vya Habari.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Haji ameandika;

Leo nimetumiwa Clip kutoka katika Radio moja ambayo baadhi ya Wachambuzi wake huitumia mara Kwa mara kunidhalilisha mimi binafsi na pia kuiponda Club ya @yangasc Kwa kila jambo.

Clip inasikika ikihoji Why kwenye Profile yangu ya Instagram nimeandika kwamba Mimi Msemaji wa Yanga ilhali nimefungiwa na TFF?

Achana na hiyo hoja dhaifu na iliyosemwa na Mtu wa hovyo hovyo, anaetumia chombo cha habari kupotosha Umma, lakini nna swali kwa Wamiliki wa kituo hicho, hivi wanajisikiaje kuona hao Wachambuzi wao kutwa kumzungumzia mtu mmoja Kwa kila baya??

Wanatumia ubinadaamu upi kukubali hilo jambo? Wanafurahi kuona hadi maisha binafsi ya Mtu yanazungumziwa ndani ya Radio yao mara Kwa mara?

Ok:: unapolalamikia eti bado nimeandika mimi msemaji wa Yanga, kwani nilichofungiwa mimi ni nini ? Sikumbuki kama TFF wamesema nimefungiwa kuajiriwa na Yanga, walichonifungia ni kutotimiza majukumu yangu, lakini hawajafungia ajira yangu.

Na ndio maana leseni ya udereva ya mtu inaweza kufungiwa na Trafik Kwa muda flani kuendesha gari, lakini haiondoi haki ya Mtu kusema yeye ni dereva na ikiwa kampuni iliyomuajiri bado inaendelea kumlipa, haki ya kujitambulisha Kwa ajira yake haizuiwi na Wahuni wa kwenye Radio, ambao wapo pale makhsuus kuponda wenzao kwa maslahi madogo wanayolipwa na Mafarisao wenzao.

Hivi kweli mimi niruhusu Manara TV iwe kila siku kuhangaika na Story za mtu mmoja tu? Tena always ni negative!! Naweza kuwacharura Simba sana kwa misingi ya utani wa jadi kwenye page hii, lakini siwezi hilo litokee Manara Tv.

Uoga wa nini kwangu wakati nimefungiwa? Ingekuwa wengine wangekuwa wanafurahia kusemwa semwa no mara waaaa! Coz kwao wanahitaji trending, lakini mimi nishavuka huko, Mimi ni pure brand katika brand zilizopo Tanzania, na ndio maana Makampuni makubwa yanawekeza kwangu katika biashara ya kujitangaza.

Haijawa kupita siku bila kunidhalilisha katika mitandao yao ya kijamii ila sijali coz kila Mtu ana njia zake za kujipatia umaarufu, lakini haikubaliki hata tone Kituo cha Redio kutumika kufedhehesha Watu kila uchwao, tena Watu wenyewe ni wale wale.

Ila Wamiliki hawajali hilo coz na wao labda wana maslahi yao kwenye hili.

SOMA NA HII  PABLO - TUMEMALIZA KAZI....WASAUZI HAWANA UJANJA TENA...