Home kimataifa GRIEZMANN AWEKWA SOKONI

GRIEZMANN AWEKWA SOKONI


 BARCELONA ipo tayari kumuuza mchezaji wao Antoine Griezmann kwa mabosi wa Chelsea ili ipate mkwanja wa kumpa nyota wao Lionel Messi kukamilisha usajili wake.

Nyota huyo hajawa kwenye mwendelezo bora ndani ya Barcelona baada ya kuibukia hapo akitokea Atletico Madrid na analipwa mkwanja mrefu.

Kwa sasa inaelezwa kuwa Chelsea ipo kwenye mpango wa kusaka mshambuliaji hivyo huenda ikamgeukia Griezmann.

Barcelona kwa sasa imezuiwa kusajili wachezaji wapya kwa kuwa imevuka kiwango cha mishahara ambayo imewekwa na La Liga hivyo lengo lao sasa ni kupunguza wachezaji.

Ikiwa itamuuza nyota huyo inaelezwa kuwa itaongeza mkwanja huo kwa ajili ya kupata saini ya Messi ambaye mkataba wake umemuguka Juni na yupo huru akiwa na timu yake ya taifa ya Argentina kwa sasa iliyotinga hatua ya fainali ya Copa America. 

SOMA NA HII  BAADA YA KUBEBA TUZO YA Ballon D'Or JUZI...BENZEMA ATAJA TIMU ATAKAYOSTAAFIA SOKA...