Home Habari za michezo SIMBA NA YANGA ZAIPANDISHA VIWANGO TANZANIA KISOKA…YAPANDA NAFASI TATU CHAP

SIMBA NA YANGA ZAIPANDISHA VIWANGO TANZANIA KISOKA…YAPANDA NAFASI TATU CHAP

Simba vs Yanga

Baada ya Klabu ya Simba SC kuifunga timu ya Horoya AC kwa bao 7-0 na kufanikiwa kuingia hatua ya robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika (CAF Champion League),

Tanzania imefanikiwa kuongeza pointi 10 na sasa kufikisha pointi 39 na kuwa na uhakika wa asilimia 100 wa kupeleka timu nne tena msimu ujao.

Aidha, baada ya Klabu ya Yanga SC kufanikiwa kuifunga timu ya US Monastir ya Tunisia jana na kuingia hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup),

Tanzania imeongeza pointi 7.5 na kufikisha pointi 46.5 na kupanda kutoka nafasi ya 9 ya Association Ranking mpaka nafasi ya saba na kulifanya Taifa kuwa miongoni mwa taifa lenye nguvu kisoka Afrika.

Point hizo 46.5 zimetengenezwa na vilabu vitatu vya Tanzania kama ifuatavyo;

10 Young Africans

35 Simba

1.5= Namungo

Ndani ya msimu mmoja Yanga imekusanya points (10) yaani. 2.5= Kufuzu makundi 7.5 = Robo fainali

Kutokana na points hizo kwa sasa Tanzania tunashika nafasi ya (7) Afrika.

1. Morocco

2. Egypt

3. Algeria

4. South Africa

5. Tunisia

6. DR Congo

7. Tanzania

Kwenye viwango vipya vya vilabu Afrika, Simba itasogea mpaka nafasi ya tisa huku Yanga itasogea hadi mpaka nafasi ya 18 na ana uwezo wa kupaa tena iwapo atafuzu nusu fainali.

SOMA NA HII  MOHAMMED HUSSEIN "TSHABALALA"...NALIAMINIA JESHI LANGU...MECHI NA UGANDA TUTASHINDA