Home Habari za michezo SIMBA WAFUNGUKA… ISHU YA KUINGIZA MASHABIKI BURE KWA MKAPA…MECHI DHIDI YA HOROYA..

SIMBA WAFUNGUKA… ISHU YA KUINGIZA MASHABIKI BURE KWA MKAPA…MECHI DHIDI YA HOROYA..

Habari za Simba
Mashabiki wa SimbaSc

Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema klabu hiyo haiwezi kufanya kiingilio bure katika mechi ya hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya Machi ya 18 ambayo ikishinda itafuzu hatua ya robo fainali.

Ahmed amesema kuna sababu mbili za kutofanya kiingilio bure kuwa ni moja, Simba ishajaza Uwanja wa Mkapa kwa kiingilio ili watu waje uwanjani na pili klabu hiyo ina mtaji mkubwa wa watu.

Amesema amepata meseji nyingi za watu wakishawishi iwe bure wakitolea mfano mechi ya Mamelodi dhidi ya Al Ahly ambayo walishinda mabao 5-2 ambalo ametolea ufafanuzi.

“Mamelodi haina mashabiki ni timu ngeni Afrika Kusini hiyo haiwezi kufanywa na Kaizer au Orlando sababu wana mashabiki wa kutosha,” amesema Ahmed

Ametaja sababu nyingine ni kuwa wakifanya mechi hiyo muhimu kuwa bure mashabiki watahoji kwanini mechi za Ligi Kuu ziwe na kiingilio.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI