Home Michezo YANGA YAMRUDISHA MATOLA CHAP

YANGA YAMRUDISHA MATOLA CHAP

YANGA YAMRUDISHA MATOLA CHAP
[the_ad id="25893"]

BAADA ya Simba Queens kutembeza kichapo cha mabao 7-0 kwa The Tigers Queens ya Arusha sasa hasira za vinara hao wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) zimehamishiwa kwenye Derby dhidi ya Yanga Princess itakayopigwa Machi 23 huku Msimbazi wakimvuta Seleman Matola kuwaongezea nguvu.

Matola, aliyeteuliwa na uongozi wa klabu hiyo kuwa mkurugenzi wa Soka la Vijana na Wanawake ameanza majukumu hayo juzi ili kusimamia Simba kutokana na mchezo mgumu uliopo kwenye mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu.

Hata hivyo, kocha huyo jana na juzi alisimamia mazoezi ya kikosi hicho kilichopo chini ya Kocha Charles Lukula, raia wa Uganda kwa lengo la kumsaidia na kesho atarejea Tanga kwa majukumu yake ya kozi ya ukocha anayosomea kwa sasa.

“Kutokana na umuhimu wa mechi hii nimeamua kumsaidia kocha kuwanoa wachezaji kwa siku mbili hizi kesho nitaendelea na majukumu yangu mengine,” alisema Matola.

Simba inayoongoza msimamo ikiwa na pointi 26 sawa na Fountain Princess zikitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa, itavaana na Yanga Machi 23 kwenye Uwanja wa Uhuru, ikiwa na kumbukumbu ya sare ya 1-1 katika mechi ya duru la kwanza. Simba inasaka taji kwa msimu wa nne mfululizo.

SOMA NA HII  KIUNGO MPYA SIMBA AMALIZA LIGI YA GHANA KWA MKOSI...SIKU YA KUTAMBULISHWA MSIMBAZI YATAJWA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here