HABARI ZA SIMBA-MPANZU
Habari za Simba Leo

KAULI YA AHMED ALLY YATHIBITISHA USAJILI WA MPANZU

Abubakar September 21, 2024 10:59 am

Winga wa zamani wa AS Vita Club Ellie Mpanzu yuko nchini kukamilisha taratibu za usajili wake na Simba, imefahamika.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amethibitisha kuwa Mpanzu yuko nchini ambapo amebainisha iwapo Simba itakamilisha usajili wake basi watakuwa wameongeza ubora kwa washambuliaji wanaotokea pembeni

“Mpanzu ni mchezaji hatari na mimi nimesikia tayari yuko jijini Dar es salaam. tunao wachezaji wazuri wa pembeni kina Edwin Mbalua, Kibu Denis, Ladack Chasambi na Joshua Mutale”

“Siku hizi pembeni kuna mchango mkubwa wa mafanikio ya kupata magoli kwa hiyo niseme wazi wachezaji wanayo nafasi ya kuboresha kiwango chao ili mwalimu awe na Imani kubwa nao”

“Kama ikitokea Tumemsajili Mpanzu basi litakuwa jambo zuri kwasababu hao vijana wote niliyokutajia bado kwa namna yake wanahitaji uzoefu kwa wakongwe kama Mpanzu,” alisema Ahmed

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Simba imebainisha kuwa Rais wa heshima Bilionea Mohammed Dewji ‘Mo’ ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ndye aliyefanikisha ujio wa Mpanzu ambapo atakamilisha usajili wake kisha ataanza kufanya mazoezi na kikosi cha Simba akisubiri dirisha dogo la usajili kufunguliwa ili asajiliwe rasmi katika mfumo

AHMED ALLY AZIPA MBINU SIMBA NA YANGA CAF ALI KAMWE…HATUJAZOEA GOLI MOJA…TUNA TIMU BORA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

One response to “KAULI YA AHMED ALLY YATHIBITISHA USAJILI WA MPANZU”

  1. […] wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba Ahmed Ally ameweka wazi kuwa bado kiwango cha Simba hakijafikia asilimia 100% inayotafutwa na Kocha Fadlu […]