Home Habari za Simba Leo AHMED ALLY AWAJIBU WANAOBEZA USHINDI WA SIMBA…UBAYA UBWELA UMEANZA KUWAINGIA

AHMED ALLY AWAJIBU WANAOBEZA USHINDI WA SIMBA…UBAYA UBWELA UMEANZA KUWAINGIA

Habari za Simba, Joshua Mutale

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba Ahmed Ally ameweka wazi kuwa bado kiwango cha Simba hakijafikia asilimia 100% inayotafutwa na Kocha Fadlu Davids.

Kila mchezaji hajafikia asilimia kubwa ya kiwango chake ikiwa ni pamoja na Leonel Ateba, Jean Ahoua huku akizungumzia na hali ya Yusuph Kagoma ambaye bado hajawa kwenye ubora wake.

“Simba hii bado yaani nyeupee kabisa itakuwa hatari.”

Lakini pia Ahmed Ally amegusia penati ya jana iliyowapa Simba Ushindi na Alama tatu muhimu akisema, ilikuwa halali na wao msimu huu wamejipanga kusambaza Ubaya Ubwela.

“Ukiwasikiliza au kusoma wanaokosoa kuwa hii sio Penati, Wanasema Mchezaji wa Dodoma Jiji alicheza mpira kwanza.

“Lakini hawazungumzii physical contact iliyofanyika hapo.

“Hawazungumziii namna Mchezaji wa Dodoma alivyomvaa Shabalala nusura amvunje mguu

Tumekariri kwamba mtu akicheza mpira kwanza kisha akacheza rafu inakua sio faulo kisa kacheza mpira kwanza.” Alisema Ahmed Ally na kuongeza;

“Hizi kelele mnazosikia wanapiga ni uoga umewaingia sasa wanatafuta huruma na visingizio Na sisi tunasema msimu huu ni kanyaga twende, Ubaya Ubwela hatusikiliza vilio vya Waombelezaji tunazika tuu.”

SOMA NA HII  NTIBANZOKIZA AMBURUZA MAYELE....SIMBA NA YANGA ZAPASUKA KICHWA