Home Habari za Yanga Leo CHADRACK BOKA ANA BALAA HUYO…YANGA ALAMA 3 KIBINDONI

CHADRACK BOKA ANA BALAA HUYO…YANGA ALAMA 3 KIBINDONI

JUMAPILI ya kufosi kwa Yanga ya Muargentina Miguel Gamondi imejibu kwa kuibuka na ushindi mbele ya KMC mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Huu ni mchezo wa kwanza kwa Yanga kucheza uwanja wa nyumbani baada

ya kucheza mechi mbili ugenini kwa kuanza na Kagera Sugar 0-2 Yanga, Ken Gold 0-1 Yanga hizi zote ilikuwa ugenini na mchezo wa nyumbani baada ya dakika 90 ubao umesoma Yanga 1-0 KMC.

Mtupiaji ni yuleyule ambaye alianza kufunga ugenini msimu wa 2024/25. Maxi Nzengeli dhidi ya Kagera Sugar amefungua pia pazia la utupiaji kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya KMC uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Ni bao la pili kwa Maxi alipachika bao hilo dakika ya 4 lilidumu mpaka mwisho wa mchezo huo ambapo KMC walicheza kwa tahadhari kubwa kuwakabili mabingwa watetezi wa ligi.

Nyota Ladrack Bocca alichaguliwa kuwa mchezaji bora ikiwa ni mara ya pili mfululizo baada ya kuwa mchezaji bora mchezo uliopita dhidi ya Ken Gold uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Yanga inafikisha pointi 9 baada ya kucheza mechi tatu na zote imeshinda huku safu ya ushambuliaji ikiwa imefunga mabao manne na ukuta haujaruhusu kufungwa ndani ya msimu wa 2024/25.

SOMA NA HII  CHADRACK BOKA ATUA BONGO USIKU WA MANANE...YANGA YAMFICHA HOTELINI

1 COMMENT

  1. […] wa kulia wa KMC, Abdallah Said ‘T Lanso’ ameeleza ugumu wa kumkaba mlinzi wa Yanga, Chadrack Boka kwamba inahitaji kutumia akili na umakini wa hali ya juu. KMC jana ilikuwa ugenini katika Uwanja wa […]

Comments are closed.