Home Habari za Simba Leo UBAYA UBWELA WATAMBA DODOMA…REFA AZUA BALAA.

UBAYA UBWELA WATAMBA DODOMA…REFA AZUA BALAA.

Klabu ya Simba imeshinda mchezo wake wa pili wakiwa ugenini kwa bao 0-1 dhidi ya wenyeji Dodoma Jiji.

Katika mchezo huo uliotawaliwa kwa kasi kubwa na ufundi wa makocha wote wawili, Fadlu kwa upande wa Simba huku Mecky Mexime kwa upande wa Dodoma mbinu zao ziliweza kuufanya mchezo huo kuwa mgumu kwa kila upande.

Pasi ndefu iliyopenyezwa na kiungo wa ball Awesu Awesu ilimkuta Zimbwe Jr ndani ya boksi kabla ya kufanyiwa madhambi na beki wa Dodoma Jiji, kisha mwamuzi akaamua kuamuru pigo la penati kwa Simba.

Jean Charles Ahoua hakufanya masihala, bali aliiandikia Simba bao la ushindi na la pekee, lililoipa klabu hiyo alama tatu Muhimu.

Mchezaji bora wa mchezo huo alikuwa ni Deborah Fernandes Mavambo, ambaye muda wote alitawala sana dimba la kati huku akisindikizwa na nidhamu kubwa.

Lakini baada ya kufungwa bao moja, vijana wa Mexime walifunguka na kuanza kusaka bao la kusawazisha ambapo mipango yao iligonga mwamba mbele ya jeshi la Fadlu Davids.

Sasa Simba imecheza mechi 4 na kushinda michezo yote, na kufunga mabao 10, huku Ahoua akihusika kwenye mabao 7 ya timu hiyo, ametoa asisti 5 na kufunga mabao 2.

Simba hadi sasa imefanikiwa kukusanya alama 12 na Clean Sheet 4.

SOMA NA HII  JINSI HALI ILIVYOKUWA...MAWAKILI WA YANGA WAKIPANGUA HOJA ZA MAGOMA MAHAKAMANI