Home Uncategorized SIMBA: YANGA WALICHEKELEA SARE YA KUFUNGANA MABAO 2-2

SIMBA: YANGA WALICHEKELEA SARE YA KUFUNGANA MABAO 2-2


MLINDA mlango namba moja wa Simba, Aishi Manula amesema kuwa wapinzani wao Yanga walifurahia sare waliyopata kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Januari 4, 2020 kutokana na kupindua meza kibabe.

Mchezo huo Yanga walikwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao 1-0 lililofungwa na Meddie Kagere na bao la pili lilifungwa na Deo Kanda kipindi cha pili.

Mabao hayo yalipinduliwa na Mapinduzi Balama baaada ya kumpora mpira Mzamiru Yassin ambaye baada ya mchezo huo hajaonekana uwanjani na bao la pili lilipatikana kupitia kwa Mohamed Issa ‘Banka’.

Manula amesema :”Wapinzani wetu walichekelea sare waliyopata hilo lipo wazi kutokana na ukweli kwamba wao walikuwa nyuma na wakapata ushindi huo wa mabao mawili ambao sisi tuliumia kuupata.

“Kwa sasa tumejipanga kwani yale yalikuwa makosa ambayo tuliyafanya tunaamini kwamba kazi itakuwa kubwa leo tutakapokutana uwanjani,” .

SOMA NA HII  ARTETA AKUBALI UWEZO WA KIPA WAKE LENO