Home Uncategorized ARTETA AKUBALI UWEZO WA KIPA WAKE LENO

ARTETA AKUBALI UWEZO WA KIPA WAKE LENO

 


MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa kia wake namba moja Bernd Leno alionyesha kiwango cha hali ya juu kwenye mchezo wa Carabao Cup uliochezwa usiku wa kuamkia leo dhidi ya Liverpool.

Mchezo huo wa raundi ya 16 uliopigwa Uwanja wa Anfield dakika 90 zilikamilika bila kufungana na kupelekea kupigwa mikwaju ya penalti ambapo Arsenal ilishinda kwa penalti 5 -4 za Liverpool.

Ushindi huo unakuwa wa pili kwa Arsenal kuishinda Liverpool kwa penalti baada ya mwezi mmoja kupita kwani ilisepa na taji la Ngao ya Jamii mwezi Agosti kwa ushindi wa Penalti 5-4.

Arteta amesema kuwa wana makipa wawili wazuri na wanaofanya kazi kwa umakini ndani ya Uwanja jambo ambalo linampa matumaini ya kufanya vizuri hatua inayofuata ambayo ni robo fainali na atakutana na Manchester City.

“Tuna makipa wawili wazuri ndani ya kikosi, wote wawili wanafanya vizuri ni suala la kufanya maamuzi nani nahitaji aanze. Leno amekuwa akitimiza majukumu yake vizuri ana kazi ya kuendelea hapo zaidi,” amesema.

SOMA NA HII  CHELSEA ZAIWINDA SAINI YA MLINDA MLANGO MANUEL NEUR