Home Habari za michezo MSHAMBULIAJI LIGI KUU AWEKA WAZI…WANASUBIRIA MIUJIZA ITENDEKE…AMEZUNGUMZA HAYA

MSHAMBULIAJI LIGI KUU AWEKA WAZI…WANASUBIRIA MIUJIZA ITENDEKE…AMEZUNGUMZA HAYA

Mwinyi Zahera Kocha wa Polisi Tanzania

MSHAMBULIAJI wa Polisi Tanzania, Ambrose Awio ameweka wazi kikosi hicho kinahitaji miujiza kubaki Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao baada ya kupoteza kwa mabao 3-0 juzi dhidi ya Singida Big Stars kwenye Uwanja wa Liti.

Akizungumza na SOKA LA BONGO, Awio alisema kwa hali ilivyo ni ngumu kwao kutokana na wengi wao kukata tamaa ila wataendelea kupambana katika michezo yao minne iliyosalia ili angalau waangukie kwenye mechi za Play-Off’.

“Kitendo cha kupoteza kinashusha sana morali ya timu na ndicho kitu ambacho kinatukumba kwa sasa, ni wazi tuna kazi kubwa ya kufanya kupata hata hiyo nafasi ya kucheza michezo ya mchujo kama hatutaongeza bidii.”

Kwa upande wa kocha msaidizi wa timu hiyo, John Tamba alisema michezo minne iliyobaki itatoa taswira yao kwa msimu huu hivyo wanahitaji kupambania pointi 12 ambazo anaamini wakizipata zitawaweka kwenye sehemu salama.

Tangu kikosi hicho ateuliwe, Mwinyi Zahera kukifundisha Desemba 2, mwaka jana kimeshinda michezo miwili tu kati ya 12 ya Ligi Kuu Bara aliyokiongoza huku minne akitoa sare na sita yote iliyosalia akichezea kichapo.

Zahera alichukua nafasi ya Mrundi, Joslin Bipfubusa aliyetimuliwa Oktoba 26, mwaka jana kutokana na matokeo mabovu na alikiongoza katika michezo saba ya Ligi Kuu akishinda pia miwili tu na kupoteza mitano.
Katika michezo 26 iliyocheza hadi sasa imeshinda minne tu, sare saba na kupoteza 15 ikiwa mkiani na pointi 19.

SOMA NA HII  MABOSI WA YANGA WAWEKA MIL 150 MEZANI...WACHEZAJI WALIPWA BONUS ZAO ZOTE