Home Ligi Kuu WAPINZANI WA YANGA WAFUNGA FEBRUARI KIBABE

WAPINZANI WA YANGA WAFUNGA FEBRUARI KIBABE

COASTAL Union ya Tanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda, Februari 28 iliifunga kibabe kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ihefu FC.

Leo ni Machi Mosi ikiwa ni siku ya awali ndani ya mwezi huu kwa mwaka 2021 ambao unazidi kwenda kasi.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga ulikuwa ni wa Kombe la Shirikisho, ambalo lipo mikononi mwa mabingwa watetezi Simba.

Imetinga hatua ya 16 bora ambapo itamenyana na wapinzani wao Mwadui Complex, Uwanja wa Mwadui Complex.

Mabao ya Coastal Union ambayo mchezo wake ujao ndani ya ligi ni dhidi ya Yanga, Machi 4 yalifungwa na Mudhathir Said dakika ya 45 na lile la pili lilifungwa na Sammy Sultan Kasikasi dakika ya 85.

Kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya 13 baada ya kucheza jumla ya mechi 21 na pointi zake ni 23 inakutana na Yanga iliyo nafasi ya kwanza na pointi zake ni 49.

  

SOMA NA HII  MSIMAMO WA LIGI KUU BARA UPO NAMNA HII KWA SASA