Home Uncategorized AJIBU APIGWA CHINI YANGA, ZAHERA AMEAMUA

AJIBU APIGWA CHINI YANGA, ZAHERA AMEAMUA


Imeelezwa kuwa Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewashangaa viongozi ya klabu hiyo kwa kuanza majadiliano ya kumpa mkataba mpya nahodha wa timu hiyo Ibrahim Ajibu.

Taarifa imeeleza kuwa Zahera amesema tangu Ajibu akatae kujiunga na TP Mazembe yeye alishamuondoa kwenye mipango yake ya msimu ujao.

Zahera ambaye kwa sasa yuko Hispania katika majukumu ya timu ya Taifa ya DR Congo inayojiandaa na fainali za AFCON 2019, ameshangaa sana kuona uongozi wa Yanga umeanza kumbembeleza nyota huyo asaini mkataba mpya.

Zahera ameenda mbali na kusema ripoti yake aliyokabidhi kwa uongozi haina jina la Ajibu na anashangaa viongozi wanamtaka Ajibu yupi wakati ameshamuondoa kwenye mipango yake.

Kwa sasa Zahera yuko Misri na kikosi cha timu ya Taifa ya Congo kwa ajili ya michuano ya AFCON inayotaraji kuanza hivi karibuni.

SOMA NA HII  ALLIANCE FC KUIFUMUA SIMBA NA YANGA