Home Uncategorized KOCHA MBELGIJI AWACHARUKIA WACHEZAJI WAKE NAMNA HII

KOCHA MBELGIJI AWACHARUKIA WACHEZAJI WAKE NAMNA HII

LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amewacharukia wachezaji wake wote wa Yanga na kuwataka wacheze kwa nidhamu mbele ya Simba leo kutokana na uimara wa wapinzani wake.
Yanga itaikaribisha Simba leo kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Taifa majira ya saa 11:00 jioni ikiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2.
Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael amesema kuwa wachezaji wake wamekuwa wakipoteza umakini wanapocheza na wapinzani wake jambo ambalo linawafanya wasifunge mabao mengi.
“Kwa sasa sina cha kuhofia mechi yetu dhidi ya Simba ila tatizo lipo kwenye safu ya ushambuliaji kushindwa kuzitumia nafasi pale wanapopata, utakuta kwenye nafasi tano ambazo tunatengeneza zote tunakosa jambo ambalo ni hatari hasa ukizingatia tunakutana na timu inayojua kufunga.
“Uwezo wao nautambua na wanajua kwamba ni namna gani wanapaswa wafanye lakini wakiwa ndani ya uwanja dakika za mwanzo wanafanya wanavyojua wao, hilo nimekaa nao nina amini wataongeza umakini,” amesema Eymael.

SOMA NA HII  YANGA WAACHANA NA JUMA ABDUL