Home Uncategorized YANGA WAACHANA NA JUMA ABDUL

YANGA WAACHANA NA JUMA ABDUL


JUMA Abdul, leo Agosti 5 ameachana na timu yake ya Yanga baada ya kushindwa kufikia makubaliano kwenye suala la mkataba wake.

Abdul ndani ya Yanga alikuwa ni nahodha msaidizi na kwa msimu wa 2019/20 amehusika kwenye jumla ya  mabao 6 kati ya 45 yaliyofungwa na Yanga akiwa ametoa pasi sita zilizoleta mabao.

Abdul amesema kuwa wameshindwa kuelewana na mabosi zake wa Yanga hasa kwa upande wa makubaliano ya mkataba wake.

“Tumeshindwa kufikiana makubaliano na Yanga kwenye upande wa mkataba wangu kwa kuwa walitaka kunipa mkataba bila ya kunilipa fedha za usajili hivyo nimeamua kuanza maisha mengine,” amesema.

Yanga ikiwa imecheza jumla ya mechi 38 ndani ya LigiKuuBara, Abdul alianza kikosi cha kwanza kwenye mechi 28.

SOMA NA HII  MZUNGU WA YANGA ATOA SOMO HILI BONGO