Home Habari za Simba Leo IMEFICHUKA MPANZU AFICHWA HOTELINI NA SIMBA…MO DEWJI AHUSIKA

IMEFICHUKA MPANZU AFICHWA HOTELINI NA SIMBA…MO DEWJI AHUSIKA

Habari za Simba- Mpanzu

WAKATI Simba inaendelea kujipanga kuwang’oa Waarabu wa Libya Al Ahli Tripoli, mabosi wa klabu hiyo wana akili nyingine kubwa na bilionea Mohammed Dewji ‘MO’ amewafanyia umafia wa maana watani wao Yanga kwa kumchukua winga mmoja hatari.

Kwa mujibu wa Mwanaspoti ni kwamba winga Mkongomani, Ellie Mpanzu yupo hapa nchini atika hoteli moja kubwa iliyopo katikati ya Jiji, amekuja kumalizana na mabosi wa Simba ili dirisha dogo likifunguliwa aliamshe Msimbazi.

Tayari makubaliano binafsi yamefikiwa,Simba wametoa $200,000 (tsh 544,740,400) Kama Sign-on fee,pia Mpanzu atalipwa $10,000 (tsh 27,237,020) kwa mwezi.

Mpanzu hakuwa kwenye mipango ya Yanga wala hakufanya mazungumzo na Yanga.

Mpanzu anatarajiwa kuitumikia Simba kwenye hatua ya makundi CAF Confederation Cup Kama watafanikiwa kuwaondoa Al Ahly Tripoli.

Ikumbukwe kaka yake Mpanzu alitua nchini mapema wiki hii kuweka mazingira sawa.

Mpanzu alihitajika zaidi na Simba dirisha kubwa la usajili, lakini alipokea mualiko wa kwenda Ubelgiji akaikacha ofa ya Simba, lakini baada ya majaribio yake kufeli huko amejikuta anaiwaza zaidi Simba kuliko kitu chochote.

SOMA NA HII  AUBIN KRAMO ATUA LIBYA...WAARABU WANAMUITA