Home Habari za Simba Leo MO DEWJI APANGA SAFU MPYA YA MASHINDANO SIMBA

MO DEWJI APANGA SAFU MPYA YA MASHINDANO SIMBA

Habari za Simba, MO Dewji

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba SC, Mohammed Dewji ‘Mo’ ameteua Kamati ya Mashindano ya klabu hiyo ambayo itakuwa na wajumbe saba.

Taarifa iliyotolewa na klabu ya Simba Agosti 1, 2024 imebainisha Wajumbe hao walioteuliwa ambao ni Mohamed Nassor, Azan Said, Richard Mwalwiba, Nicky Magarinza, Juma Pinto, Farid Nahdi na Farouk Baghozah.

Hawa ni Wajumbe ambao watahakikisha Kila kitu kinakwenda sawa ndani ya klabu hiyo, ikiwemo kurejesha Ubingwa na ubabe kwenye Soka la Tanzania na Afrika.

Simba haijachukua ubingwa wa Ligi Kuu kwa misimu mitatu sasa,  huku  ubingwa wa Kombe la Shirikisho wakiwa hawan chochote kwa misimu 3 pia.

Msimu  huu Simba imefanya usajili wa wachezaji wengi sana, hivyo kikosi chao ni kipya  kwa sasa.

Wachezaji waliosajil na Simba kwa msimu huu wa 2024/25 ni Joshua Mutale, Steve Mukwala, Jean Ahoua,  Chamou Karaboe, Valentin Nouma, Augustine Okejepha, Deborah Fernandes, Valentine MASHAKA, Abdurazak Hamza, Mlinda mlango Mpya Moussa Camar, Klvin Kijiri, Awesu Awesu, Omary Adam.

SOMA NA HII  KOCHA WA TAIFA STARS...AWATAFUTA KAPOMBE NA TSHABALALA