Home Habari za michezo SIMBA NA YANGA WANA JAMBO LAO WIKIENDI HII.

SIMBA NA YANGA WANA JAMBO LAO WIKIENDI HII.

Habari za Simba na Yanga

WIKIENDI hii Yanga na Simba zina mechi za kuamua hatma zao katika michuano ya kimataifa kila mmoja akipambania rekodi zake.

Wakati wakipambania rekodi, kuna matumaini makubwa yapo kuanzia kwa wachezaji, viongozi, makocha hadi mashabiki, asilimia kubwa ya kutoboa ipo wazi.

Jeuri hiyo inakuja kufuatia rekodi nzuri walizonazo wawakilishi hao wa Tanzania waliosalia katika michuano ya kimataifa msimu huu.

Kesho Jumamosi, Yanga inacheza mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CBE SA ya Ethiopia baada ya ugenini kushinda 1-0 na imeupeleka Zanzibar kwenye Uwanja wa New Amaan Complex ukitarajiwa kuchezwa saa 2:30 usiku.

Simba yenyewe itacheza Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam sehemu ambayo wamekuwa wakijiona ni salama zaidi kwao linapokuja suala la mechi za kimataifa.

Hapa Simba itapambana na Al Ahli Tripoli ya Libya ukiwa ni mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ugenini matokeo kuwa 0-0.

SOMA NA HII  HUYU HAPA MSAIDIZI WA AUCHO YANGA