Home Habari za Simba Leo MECHI YA SIMBA VS AL AHLI REKODI ZINAMBEBA MNYAMA

MECHI YA SIMBA VS AL AHLI REKODI ZINAMBEBA MNYAMA

Uwanja wa Mkapa

Katika misimu sita iliyopita, Simba walikuwa na rekodi ya kuvutia wakiwa nyumbani katika michezo ya maamuzi kabla ya kutinga makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba imekwama mara moja tu, ikiwa kwa Mkapa katika mechi za maamuzi ili kutinga makundi ya Ligi ya Mabingwa, jambo linaloonyesha uthabiti na uwezo wa kukabiliana na viunzi vya hatua hiyo.

Msimu wa 2018-19 ulikuwa wa kihistoria kwa Simba. Baada ya kushindwa na Nkana kwa mabao 2-1 ikiwa ugenini Zambia, ilirejea kwa kishindo Kwa Mkapa na kuwachakaza wapinzani kwa mabao 3-1.

Ushindi huo haukuwa wa kawaida, kwani ulionyesha ujasiri wa Simba na uwezo wa kupindua matokeo. Msimu huo, Simba iliendelea kucheza kwa kiwango cha juu hadi kufikia robo fainali, rekodi ambayo bado inasalia kuwa moja ya mafanikio makubwa kwa klabu hiyo katika michuano ya Afrika.

Hata hivyo, msimu wa 2019-20 ulikuja na changamoto zake. Simba, chini ya kocha Patrick Aussems, walijikuta wakitupwa nje ya michuano hiyo na UD Songo ya Msumbiji tena hatua za awali walishinda hata kufika katika mechi za maamuzi.

Baada ya sare tasa ugenini, Simba walishindwa kutumia vyema uwanja wa nyumbani walipotoka sare ya 1-1 na kutolewa kwa kanuni ya bao la ugenini. Ni pigo lililowafanya Simba kuelewa kuwa michuano ya Afrika inahitaji nidhamu na umakini wa hali ya juu.

Simba walifanya maboresho makubwa msimu uliofuata (2020-21). Usajili wa Luis Miquissone kutoka UD Songo ulikuwa na mchango mkubwa katika kuibeba timu hiyo, hasa katika mchujo dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe.

Baada ya kupoteza 1-0 Zimbabwe, Simba walirejea kwa kishindo katika Uwanja wa Mkapa na kuwachapa wapinzani kwa mabao 4-0, ushindi uliowafikisha hatua ya makundi.

Msimu wa 2021-22 ulikuwa na machungu kwa mashabiki wa Simba. Baada ya ushindi mnono wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana, wengi walidhani kuwa tiketi ya hatua ya makundi ilikuwa tayari mfukoni.

Hata hivyo, mchezo wa marudiano ulileta mshangao mkubwa baada ya Simba kuchapwa mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Mkapa na kutupwa nje ya michuano hiyo. Pigo hilo lilikuwa fundisho kwa Simbana walijitathmini na kurejea kwa nguvu katika michuano mingine, wakifika robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Katika misimu miwili ya hivi karibuni (2022-23 na 2023-24), Simba wameonyesha ujasiri na nidhamu ya hali ya juu kwenye mechi za maamuzi.

Ushindi dhidi ya C.D. Primeiro de Agosto ya Angola walishinda bao 1-0 nyumbani (ushindi wa jumla 4-1) na Power Dynamos walitoa sare ya 1-1 nyumbani walipita kwa kanuni ya mabao ya ugenini, mechi ya kwanza walitoka 2-2

SOMA NA HII  CHAMA AWAPA SIMBA FILE HILI LA MZAMBIA ...KILA KITU SHWARI